Elimu ya Majini
Majini ni viumbe walioumbwa kabla ya binadamu na wana mifumo miwili tofauti: Wengine ni wema na hawana madhara kwa wanadamu. Wengine ni wabaya na wanaweza kuleta madhara. Pia kuna wanyama walioko katika makundi mawili: Wanyama wa porini ambao si rafiki kwa wanadamu. Wanyama wa kufugwa wanaoweza kuishi na wanadamu. Vivyo hivyo, majini hujumuisha wale wanaopenda kusaidia na wale wanaopenda kuharibu. Katika elimu hii, nitafundisha jinsi ya kujikinga na majini wabaya na kupata mafanikio kupitia maarifa haya. Kabla ya kuanza, hakikisha umejiunga (subscribe) kwa mwendelezo wa elimu hii. Majini ni viumbe walioumbwa kabla ya binadamu, kama ilivyoelezwa kwenye vitabu mbalimbali vya elimu ya majini. Wameumbwa na Mungu kwa mifumo tofauti, wengine wakiwa waovu na wengine wema. Katika historia ya uumbaji, malaika waliumbwa kabla ya majini, na baadaye binadamu wakaumbwa. Majini wanaweza kuathiri maisha ya wanadamu, hivyo ni muhimu kujifunza kuhusu wao ili kujikinga na madhara...